わたしの『やめて』 » ‘Sitaki’

Vita ni ugomvi baina ya nchi na nchi.

Vita vinaanza kwa kisingizio cha watu kwamba “nitakuua wewe kabla ya mimi.”
Vita vinaongeza faida kwa wauzaji silaha.
Vita vikianza, hakuna mtu anayeweza kuvisimamisha.

Kuanza vita ni rahisi, lakini kumaliza vita ni vigumu.
Vita vinawapa mateso wanajeshi, wazee na watoto pia.
Vita vinachana mikono, miguu na vinararua moyo wa watu pia.

Moyo wangu ni wangu.
Sitaki mtu acheze na moyo wangu.
Maisha yangu ni yangu.
Sitaki kuwa silaha ya watu.

Bahari ni pana, lakini si pahala pa kujenga kambi za vita.
Anga ni pana, lakini si pana kwa kurushia ndege za vita.

Mimi sitakubali kuwamo katika vita na kuwaumiza watu, nataka kuwapa moyo wale waliojeruhiwa.

Hatusomi shule kwa maana ya kutengeneza silaha.
Hatusomi shule kwa maana ya kupata pesa nyingi.
Hatusomi shule kwa maana ya kusikiliza wanavyosema wengine.

Ninataka kuthamani maisha yangu na ya watu wengine, halafu ninataka kufikiria na kuzungumuza mambo tunayoyapenda wakati wowote.
Lakini vita vinatuzuia tusifanye mambo tunayoyapenda.

Kwa hivyo ninataka kuwaambia kwa sauti kubwa kwa watu wanaotaka kuanza vita ‘Sitaki’.

Kampeni kwa Uhuru na Amani ya Chuo Kikuu cha Kyoto