声明書 » WITO

Vita vinaanza katika mwamvuli wa kujilinda.
Vita vinazinufaisha sekta za kutengeneza silaha.
Vita mara vinapoanza havidhibitiki kirahisi.

Vita ni rahisi kuanza kuliko kuvimaliza.
Vita si vinawaletea balaa askari-vita tu bali wazee na watoto pia.
Vita si vinawadhuru binadamu mikono na miguu yao tu bali madhara yake yanapenya ndani ya mioyo yao pia tena na zaidi.

Utu wa mtu si kitu cha kudhibitiwa na wengine.
Utashi ni wake mwenyewe si wa mwingine.

Bahari isielemewe na ngome za kijeshi.
Mbingu isinajisiwe na ngurumo za ndege za kijeshi.

Tunataka kuishi katika nchi ya kipekee inayosifu kuzalisha hekima kuliko nchi ya kawaida tu inayoona kujitolea kupigana na wengine ni michango.

Utaalamu si silaha ya vita.
Utaalamu si nyenzo ya biashara.
Utaalamu si mtumwa wa mwenye nguvu.

Ili kulinda na kujenga pahala pa kuishi na uhuru wa kufikiri,
sisi, kwa dhati yetu, lazima tuipinge vikali nguvu yenye kiburi.

Kampeni kwa Uhuru na Amani ya Chuo Kikuu cha Kyoto